Tazama Video: MASHABIKI WA COASTAL UNION WAKIMSHAMBULIA MWAMUZI THOMAS MKOMBOZI

Tukiwa tunasubiri hatma ya Coastal Union leo kwa Kamati ya saa 72 kuketi kujadaili ripoti za mchezo ambao Mashabiki wa timu ya Coastal Union walipompiga mwamuzi Thomas Mkombozi alipokuwa akichezesha mchezo wa Coastal na KMC.
Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, amesema pamoja na kusubiria maamuzi ya kamati hiyo, kanuni za wazi ni kwamba iwapo ripoti zitabainisha mashabiki ndio wenye makosa, basi Coastal kuna hatari ya kucheza mechi zilizobaki bila mashabiki ama kuhamishwa kutoka uwanjani hapo.
Share: