Taarifa hizo ambazo Esma mwenye alizikanusha zinaeleza kuwa wawili hao hukutana kwa siri kwa sababu wanataka uhusiano wao huo uwe ni siri kwao tu.
Ivan Ssemwanga
Akizungumaza na gazeti la Kiu, Esma Platnumz alisema kuwa hakuna mtu
yeyote anayeweza kumpangia nani wa kuwa rafiki yake na nani asiwe.
Alieleza kuwa yeye ni mke wa mtu na anaiheshimu ndoa yake na kama kuna
chochote wanachodhani kuwa kipo kati yake na Ivan wanapoteza muda kwani
Ivan ni rafiki yake tu.Baadhi ya watu wamedai kuwa kama kuna chochote kati ya Esma Platnumz na Ivan basi itakuwa ni kisasi kwa Diamond Platnumz kumchukua aliyekuwa mke wa Ivan, Zari the Boss Lady.