Katika
majibizano hayo, pia polisi walidai kukamata bendera zenye maandishi ya
lugha ya Kiarabu, redio saba za upepo na soksi za kuficha nyuso.
Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo wa Polisi, Nsato Marijani alisema jana kuwa
hiyo ilikuwa operesheni ya kuwasaka majambazi waliovamia Chuo Kikuu cha
Sekomu, wilayani humo hivi karibuni.
Alisema
katika tukio hilo, askari wawili walijeruhiwa kwa risasi. Marijani
ambaye alikuwa katika milima hiyo inayodaiwa kuwa ngome ya majambazi
hao, aliwataja waliouawa kuwa ni Mudrick Abdi (24) maarufu kwa jina la
Osama, mkazi wa Mbagala Majimatitu Dar es Salaam na Sultan Abdallah (24)
mkazi wa Kiembesamaki, Zanzibar.
Alisema
askari waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu na kwamba hawakupata
madhara makubwa kwa kuwa walikuwa wamevaa majaketi ya kuzuia kupenya
risasi .